Sunday, 12 March 2017

Dhambi ya asili (au dhambi asili) ni jinsi Wakristo wa madhehebu mbalimbali wanavyoita dhambi ya kwanza ya watu ambayo imekuwa asili ya dhambi zote (Rom 5:12) na ya uharibifu wa tabia ya binadamu na ya dunia kwa jumla (Rom 8:19-25).

Dhambi ya asili katika Biblia

Michelangelo alivyochora katika kuta za Cappella Sistina huko Vatikano dhambi ya Adamu na Eva naadhabu iliyofuata ya kufukuzwa bustanini.
Kitabu cha Mwanzo sura ya 3 inasimulia dhambi hiyo. Kwa njia ya
 hadithi hiyo tunaambiwa hali mbaya ya binadamu haitokani na Mungu moja kwa moja, bali na uasi wetu na wa wazee wetu (Hek 2:23-24). Pia tunafundishwa kukataa toka mwanzo vishawishi vyetu tukiamini maagizo yote ya Mungu yametolewa naye kwa upendo mkuu.
Shetani ndiye aliyeanzisha kishawishiEva alipaswa asimsikilize. Kosa lake la kwanza ni kumjibu: hivyo shetani akamdanganya kwamba, eti Mungu ana kijicho, hataki watu walingane naye, ndiyo sababu aliwakataza (Yoh 8:44). Tukianza kuzingatia kishawishi tunakubali shaka juu ya wema wa Mungu kwetu katika kutuelekeza. Kwa namna hiyo walianguka watu wa kwanza waliokuwa watakatifu; kwa urahisi zaidi tutaanguka sisi wenye tabia mbaya kutokana na dhambi hiyo na nyingine nyingi.
Hata baada ya dhambi Mungu anamtafuta mtu kwa upendo, ila huyo kwa aibu anamkimbia, au akijisikia analaumiwa nadhamiri, basi anatafuta visingizio hata kumlaumu Mungu kana kwamba ndiye aliyesababisha. Kwa utakatifu wake Mungu hawezi kuvumilia maovu, na kwa haki yake anataka makosa yalipwe. Ndiyo sababu tunakuta matatizo maishani, kama vile uchungu wa uzazi, kuhusiana kwa mabavu, kupata riziki kwa shida, na hasa kufa: hayo yote ni matokeo ya dhambi.
Pamoja na hayo Mungu hapendi mtu yeyote apotee (2Pet 3:9), hivyo toka mwanzo aliahidi kwamba mzawa wa Eva atamponda kichwa shetani (Mwa 3:15). Ndiyo habari njema ya awali kuhusu wokovu ujao
SOURCE:https://sw.wikipedia.org/wiki/Dhambi_ya_asili

No comments:

Post a Comment